728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    LIGI KUU BARA KUENDELEA TENA LEO,KESHO,JE STAND UNITED KUISIMAMISHA YANGA LEO???

    Shinyanga,Tanzania.

    Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea tena leo Mei 3,2016 kwa mchezo mmoja ambao Mabingwa watetezi Yanga ya Dar es Salaam watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

    Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na timu zote mbili kupata matokeo tofauti katika michezo yao ya wikendi iliiyopita.

    Stand United iliangukia pua kwa kuchapwa mabao 2-1 na Mwadui FC huku Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wao waliichapa Toto Africans kwa mabao 2-1 huko CCM Kirumba,Mwanza.

    Ushindi katika mchezo wa Leo utakuwa umeisogeza Yanga karibu kabisa na ubingwa wa pili mfululizo kwani itakuwa imefikisha pointi 68 na kuviacha mbali vilabu vya Azam FC na Simba SC ambavyo vinafuatia vikiwa na pointi 59 na 58.

    Jumatano Mei 4, 2016 Ligi hiyo itaendelea tena kwa mchezo mmoja kupigwa: Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

    Michezo hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA KUENDELEA TENA LEO,KESHO,JE STAND UNITED KUISIMAMISHA YANGA LEO??? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top