728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    YANGA SC YAENDELEA KUVUNA POINTI KANDA YA ZIWA ,YAICHAPA STAND UNITED 3-1CCM KAMBARAGE

    Shinyanga,Tanzania.

    MABINGWA watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga SC wameendelea kuvuna pointi kanda ya ziwa baada ya jioni ya leo kuichapa Stand United kwa mabao 3-1 katika mchezo pekee uliochezwa katika uwanja wa CCM Kambarage,Shinyanga.

    Yanga SC ilianza kujipatia bao la kuongoza mapema tu dakika ya 2 kupitia kwa Donald Ngoma baada ya walinzi wa Stand United kujisahau.Dakika ya 44 Ngoma aliifungia Yanga SC bao la pili baada ya kuiwahi pasi ndefu ya Hamis Tambwe na kufikisha mabao 16 Ligi Kuu.

    Yanga SC ilipata bao la tatu dakika ya 63 kipitia kwa Hamisi Tambwe aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Simon Msuva na kufikisha mabao 20 Ligi Kuu.

    Dakika ya 81 Stand United ilipata bao kupitia kwa Elias Maguli aliyefunga kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Thabani Kamusoko kumwangusha kwenye eneo la hatari mchezaji mmoja wa Stand United.

    Kwa matokeo hayo Yanga SC imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 68 na kujihakikishia kuutetea ubingwa wake ilioutwa msimu uliopita.

    Kesho Jumatano Mei 4,2016 Azam FC itakuwa nyumani Azam Complex,Chamazi kuialika JKT Ruvu ya Pwani.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAENDELEA KUVUNA POINTI KANDA YA ZIWA ,YAICHAPA STAND UNITED 3-1CCM KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top