728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 04, 2016

    UCL:GRIEZMANN AIPELEKA FAINALI ATLETICO MADRID,KAZI YABAKI KWA RONALDO NA AGUERO LEO

    Munich,Ujerumani.

    Atleco Madrid imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya Jumanne Usiku kuchapwa mabao 2-1 na Bayern Munich katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili uliochezwa katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich.

    Wenyeji Bayern Munich ndiyo walianza kupata bao katika dakika ya 31ya kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wake Xabi Alonso.

    Lakini Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico Madrid baada ya kugongeana vizuri na mkongwe Fernando Torres.

    Dakika ya 74 Robert
    Lewandowski aliifungia Bayern Munich bao la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Arturo Vidal na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka mwisho wa mchezo.

    Hii ina maana kwamba Atletico Madrid imesonga kwenda fainali kwa faida ya bao la ugenini baada ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata Jumatano ya wiki iliyopita ikiwa nyumbani Vicente Calderon,Madrid kwa bao la maajabu la Saul Niguez.

    TIMU ZOTE ZAKOSA PENATI

    Kila timu ilikosa penalti Bayern Munich ndiyo ilikuwa ya kwanza kukosa penati baada ya mlinda mlango Jan Oblak kucheza penati ya Thomas Muller na upande wa Atletico, Fernando Torres naye akakosa baada ya penati yake kuchezwa na mlinda mlango Manuel Neuer.

    Nusu fainali ya pili itachezwa leo Jumatano,Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kuialika Manchester City na mashindi ataungana na Atletico Madrid kuchezo fainali huko San Siro,Italia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCL:GRIEZMANN AIPELEKA FAINALI ATLETICO MADRID,KAZI YABAKI KWA RONALDO NA AGUERO LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top