728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    TOTTENHAM YAWEKA REKODI YA UTOVU MKUBWA WA NIDHAMU LIGI KUU ENGLAND.

    London,England.

    Tottenham imeweka rekodi ya utovu mkubwa wa nidhamu baada ya Jumatatu usiku wachezaji wake tisa kulimwa kadi za njano katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya Chelsea ulioisha kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

    Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Stamford Bligde licha ya wachezaji wa pande zote mbili kuchezeana kibabe lakini Tottenham ndiyo iliyokuwa na bahati mbaya zaidi baada ya wachezaji wake tisa kulimwa kadi za njano kwa mchezo mbaya ambayo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu England.

    Wachezaji hao ni Jan Vertonghen,Danny Rose, Kyle Walker, Eric Dier, Mousa Dembele, Erik Lamela, Christian Eriksen,Harry Kane na Ryan Mason. Chelsea wao waliambulia kadi tatu pekee za Branislav Ivanovic, John Obi Mikel na Willian.

    Hii ina maana kwamba Tottenham itatozwa faini kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake huku kiungo wake Moussa Dembele akikabiriwa na adhabu kali toka FA kwa kosa la kumjeruhi jichoni  mshambuliaji wa Chelsea Muhispania Diego Costa.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TOTTENHAM YAWEKA REKODI YA UTOVU MKUBWA WA NIDHAMU LIGI KUU ENGLAND. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top