Ng'olo Kante
Kante:Manchester United wako tayari kutoa £30m kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Leicester City Mfaransa N’Golo Kante.Kante,25 alijiunga na Leceister City mwezi Juni akitokea Caen kwa kitita cha £8m.(Daily Star)
Bale:Jina la Gareth Bale limeibukia katika orodha ya nyota wanaowindwa na Manchester City lakini Real Madrid inaamini nyota huyo wa zamani wa Tottenham atasaini mkataba mpya na kubaki Santiago Bernabeu mpaka mwaka 2021. (Sunday Express)
Van Gaal:Kocha wa Manchester United Mholanzi Louis van Gaal amesisitiza kuwa bado ataendelea kukinoa kikosi hicho licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa atafukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.( Mail on Sunday)
Ranieri:Leicester City itaanza maandalizi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao kwa kuwazawadia mikataba mipya kocha wake Claudio Ranieri na winga wake Riyad Mahrez.( Sunday Telegraph)
Rudiger: Cheslea inataka kuongeza nguvu katika safu yake ya ulinzi kwa kumsajili mlinzi wa kati wa Stuttgart anayechezea Roma kwa mkopo Antonio Rudiger,23.Mlinzi huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Ujerumani ana thamani ya €9m.(Corriere dello Sport)
Mascherano:Juventus wameripotiwa kufikiria kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona Javier Mascherano lakini kipengele cha mauzo cha €100m kilichopo katika mkataba wa Muargentina huyo kimeripotiwa kuwa kitaikwamisha klabu hiyo ya Italia.(Sport)
Lewandowski:Arsenal imeripotiwa kuwa itakuwa tayari kuingia katika mbio za kutaka kumsajili Robert
Lewandowski ikiwa mshambuliaji huyo toka Poland ataamua kutimka Bayern Munich.Arsenal imeandaa kitita cha £150m kwa ajili ya kusajili nyota wapya pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa.(Daily Mirror)
Ibrahimovic:Juventus wameripotiwa kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Paris Saint Germain Zlatan Ibrahimovic baada ya kudaiwa kumwandalia mshahara wa €7m kwa mwaka.(Sport Mediaset)
Oxford:Kocha mpya wa Manchester City Muhispania Pep Guardiola anataka kumsajili mlinzi kinda wa West Ham Reece Oxford kwa ajili ya kuongeza wachezaji wazawa katika kikosi chake.(Daily Mail)
Lemar:Liverpool imeripotiwa kutaka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kumsajili kinda wa Monaco Thomas Lemar,20.(Daily Star)
Benati:Arsenal inataka kumsajili mlinzi wa kati wa Bayern Munich Mmorocco Mehdi Benatia hii ni baada ya nahodha Per Mertesacker kuwa mbioni kutimka klabuni hapo.(Starsport)
Townsend:Southampton imetajwa kutaka kumsajili winga machachari Andros Townsend ikiwa tu klabu yake ya Newcastle United itashuka daraja.( The Sun)
Benati:Arsenal inataka kumsajili mlinzi wa kati wa Bayern Munich Mmorocco Mehdi Benatia hii ni baada ya nahodha Per Mertesacker kuwa mbioni kutimka klabuni hapo.(Starsport)
0 comments:
Post a Comment