Ayew aakishangilia bao
Swansea,Wales.
Swansea City imefuta uteja wa muda mrefu baada ya mchana wa leo kuichapa Liverpool kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliopigwa katika uwanja wa Liberty huko Wales.
Swansea City imepata mabao yake kupitia kwa Mghana Andrew Ayew aliyefunga mabao mawili dakika za 20 na 67 na Jack Cork dakika ya 33 huku lile la Liverpool likifungwa na Christian Benteke dakika ya 65.
Dakika ya 76 Liverpool ilipata pigo baada ya mlinzi wake Brad Smith kulimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.
0 comments:
Post a Comment