Barcelona,Hispania.
Huwezi kuamini lakini huu ndiye ukweli wenyewe.Dani Alves ni zaidi ya Pele!!
Ubingwa wa 24 wa La Liga iliyoutwaa FC Barcelona jana Jumamosi baada ya kuichapa Granada kwa mabao 3-0 huko Estadio Nuevo Los Carmenes umemfanya mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Daniel Alves da Silva kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Brazil kutwaa mataji mengi zaidi katika historia ya taifa hilo.
Ubingwa huo ambao ni wa sita wa La Liga kwa Alves,33 akiwa na FC Barcelona umemfanya afikishe mataji 30 ikiwa ni taji moja zaidi ya Pele mwenye mataji 29 yakiwemo mataji matatu ya dunia aliyotwaa na timu ya taifa ya Brazil.
Alves anaweza kuiongeza tena rekodi hiyo na kufikia 31 kiwa FC Barcelona itatwaa ubingwa wa Copa del Rey Jumapili ijayo itakapoumana na Sevilla katika mchezo wa Fainali.
Kama hiyo haitoshi Alves ameingia katika rekodi nyingine tena kwani pasi aliyoitoa kwa Luis Suarez na kuipatia FC Barcelona bao la pili imemfanya mlinzi huyo wa zamani wa Sevilla afikishe pasi (Assists) 100 za mabao La Liga na kuwa mchezaji wa tatu kufikia idadi hiyo baada ya Lionel Messi na Luis Figo.
Pele enzi za ujana wake
0 comments:
Post a Comment