Barcelona,Hispania.
Mlinzi wa Arsenal Hector Bellerin ametwaa tuzo ya mchezaji bora kinda wa mwaka wa jimbo la Catalunya,Barcelona.
Bellerin,20 ameibuka kidedea baada ya kupata asilimia 57 ya kura zote zilizopigwa,nafasi ya pili imeenda kwa Pau Lopez wa Espanyol aliyepata asilimia 30 huku Keita Balde wa Lazio akipata asilimia 13.
Tuzo hii hutolewa na chama cha soka cha jimbo la Catalunya (CFC) kila mwaka kwa wachezaji wazawa ambao wanakuwa wamefanya vizuri katika ligi mbalimbali.
Mbali ya Bellerin nyota wengine waliotwaa tuzo usiku wa jana ni Gerrard Pique aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora kwa jumla huku Jonathan Soriano wa Red Bull Salzburg akiibuka akiibuka kinara kwa upande wa upachikaji mabao.
0 comments:
Post a Comment