728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, November 10, 2015

    SIMBA YAGOMA KUMUACHIA KESSY,YATOA KAULI NZITO KWA YANGA NA AZAM


    BAADA ya Azam na Yanga kutangaza kumuwania beki wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na kutoa kauli nzito juu ya mchezaji wao huyo.

    Akizungumza jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema Kessy haendi kokote kutokana ni mchezaji halali wa Simba.

    Manara alisema bado wana mkataba na beki huyo na hawana mpango wa kumwacha katika kipindi hiki cha usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaofunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka huu.

    Alisema beki huyo anaendelea kuichezea klabu hiyo na kamwe hawatamruhusu kujiunga na klabu nyingine kwa kuwa bado ana mkataba na Simba.


    Manara ameibuka na kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba Azam na Yanga wanawania saini ya beki huyo ili waweze kuviimarisha vikosi vyao kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
    Ilielezwa kwamba, Yanga wameanza kufanya mipango ya chini kwa chini katika kuhakikisha wanampata beki huyo ambaye atakuja kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.
    Yanga ambayo ilihusishwa na mchezaji huyo katika usajili uliopita, imeelezwa kufika mbali katika kufanikisha zoezi la usajili wa beki huyo licha ya kufanya mambo yake chini kwa chini.
    Manara alisema zinaweza kuwepo taarifa katika hilo lakini suala la Simba kumuachia Kessy wakati ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chao hilo halipo na wanaofikiria hivyo basi ni bora wafute mawazo hayo kwani Simba pia inahitaji kuimarika.


    (Chanza:Gazeti la Bingwa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA YAGOMA KUMUACHIA KESSY,YATOA KAULI NZITO KWA YANGA NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top