Manchester, England.
Nahodha wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ubelgiji Vincent Kompany amefichua kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa ataikosa michuano ijayo ya kombe la Ulaya [Euro 2016] inayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa mwezi Ujao.
Kompany,30 ataikosa michuano hiyo kufuatia jeraha la misuli alilolipa katika mchezo wa Jumatano wa Ligi ya Mabingwa ambao uliisha kwa klabu yake ya Manchester City kuchapwa bao 1-0 na Real Madrid katika mchezo wa pili wa nusu fainali.
Katika mchezo huo uliochezwa huko Santiago Bernabeu Kompany alidumu uwanjani kwa dakika tano tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Eliaquim Mangala.
Jeraha hilo ni la tano kwa Nahodha huyo ndani ya msimu huu.Kompany ameichezea Manchester City michezo 22 pekee kati ya 57 iliyocheza klabu hiyo ya Etihad.
Kwa maana hiyo jukumu la kuiongoza Ubelgiji katika michuano ya Euro limekwenda kwa nahodha msaidizi Eden Hazard.Ubelgiji iko kundi E pamoja na mataifa ya Italia, Ireland na Swedeni.
0 comments:
Post a Comment