728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    LEWANDOWSKI AWEKA REKODI NYINGINE BUNDESLIGA,ASAKA NYINGINE

    Munich,Ujerumani.

    Robert Lewandowski ameifikia rekodi ya Mdachi Klaas-Jan Huntelaar ya kufunga mabao 29 katika msimu mmoja wa Ligi ya Bundesliga idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa na mchezaji asiye raia wa Ujerumani.

    Lewandowski,27 ambaye ni raia wa Poland aliiweka rekodi hiyo jana Jumamosi pale alipoifungia Bayern Munich mabao yote mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ingolstadt na kurudia kile alichokifanya Huntelaar msimu wa 2011-12 akiwa na Schalke.

    Lewandowski bado ana nafasi ya kumpiku Huntelaar na kuweka rekodi ya peke yake ikiwa atafunga katika mchezo wa mwisho ambao Bayern Munich itakuwa nyumbani Allianz Arena kucheza na Hannover 96 ambayo tayari imeshashuka daraja.

    Pia Lewandowski amekuwa mchezaji wa kwanza wa Bayern Munich kufunga mabao 29 katika msimu mmoja wa Bundesliga 
    tangu Karl-Heinz Rummenigge afanye hivyo msimu wa 1980-81.

    Ushindi huo wa Jumamosi umeifanya Bayern Munich ichukue ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya nne mfululizo.

    Picha chini ni Klaas-Jan Huntelaar


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LEWANDOWSKI AWEKA REKODI NYINGINE BUNDESLIGA,ASAKA NYINGINE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top