728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    ANYOLEWA NYWELE LIVE KWENYE TV KISA KUIBEZA LECEISTER CITY

    Cairo, Misri. 

    KAUMBUKA!!Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Tottenham,Ajax,Marseille,Roma, Middlesbrough,West Ham na timu ya taifa ya Misri Ahmed Hossam maarufu kama ‘Mido’ amejikuta akipata aibu ya mwaka kisa kubeza ubingwa wa Leceister City.

    IMEKUWAJE?? 

    Mido,33 ambaye kwa sasa anafanya kazi ya mchambuzi wa soka katika kituo cha Televisheni cha beIN Sports mapema mwezi Januari alisema licha ya Leceister City kuwa kileleni mwa msimamo wa eti isingeweza kutwaa ubingwa wa England na badala yake itapokonywa nafasi hiyo na klabu yake ya zamani ya Tottenham.

    Mido alikwenda mbali zaidi na kuhaidi kuwa ikiwa Leicester City watatwaa taji la Ligi Kuu basi atanyoa nywele zake ambazo zimekuwa kama ndio utambulisho wake.

    Ahadi ni deni huyu hapa Mido akitimiza ahadi ya kunyolewa nywele tena Live kwenye Televisheni.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ANYOLEWA NYWELE LIVE KWENYE TV KISA KUIBEZA LECEISTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top