728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    BONDIA AMIR KHAN ADUNDWA KWA KO

    Bolton,Uingereza.

    Bondia wa Uingereza Amir Khan leo alfajiri amepoteza mchezo wa kuwania taji la WBC uzito wa kati baada ya kudundwa kwa KO katika raundi ya sita na Mmexico Saul Canelo.

    Khan mzaliwa wa Bolton,Uingereza aliuanza vyema mpambano huo uliopigwa katika ukumbi wa T-Mobile Arena kwa kumshambuliaji Canelo kwa makonde mazito mazito.

    Ilipofika raundi ya sita kibao kikageuka,Khan akaanza kupoteza makali na kumuachia mwanya Canelo ambaye alianza kuvurumisha makonde makali makali mithiri ya radi na kumpeleka Khan chini akiwa hajitambui hali iliyofanya mwamuzi Kenny Bayless amalize mpambano huo ili kunusuru maisha ya bondia huyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BONDIA AMIR KHAN ADUNDWA KWA KO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top