MABINGWA mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamesitisha mpango wa kuja Dar es Salaam kuweka kambi fupi kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hiyo yenye Watanzania wawili, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ilitaka kuja Dar es Salaam wiki hii kwa maandalizi ya mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Al Hilal nchini Sudan Jumapili ya Agosti 23, lakini imeghairi.
Habari za ndani zinasema kwamba Mazembe ilitaka kuja kwa siri Dar es Salaam, lakini baada ya habari za ujio wao kuvuja, wameamua kughairi kwa kuhofia hujuma za wapinzani wao.
0 comments:
Post a Comment