Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney ataukosa mchezo wa leo wa ligi kuu England dhidi ya Liverpool baada ya kupata majeraha ya misuli ya mguu.
Rooney hakuwepo katika mazoezi ya mwisho jana ijumaa katika uwanja wa mazoezi wa AON Training Complex na pia hakuwa katika kikosi cha wachezaji 18 kilichofika katika hoteli ya Lowry kuweka kambi fupi.
Kufuatia kukosekana kwa Wayne Rooney kocha Luis Van Gaal anatarajiwa kuziba pengo hilo kwa kutumia kiungo Marouane Fellaini ama mshambuliaji kinda toka Monaco Anthony Martial.
Wachezaji 18 waliowasili katika hoteli ya Lowry ni: Sergio Romero, David De Gea, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Chris Smalling, Paddy McNair, Daley Blind, Marcos Rojo, Luke Shaw, Ander Herrera, Michael Carrick, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Marouane Fellaini, Memphis Depay, Juan Mata, Ashley Young and, Anthony Martial.
0 comments:
Post a Comment