Wakati ligi kuu ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo jumamosi kwa timu kujitupa viwanjani kusaka pointi tatu muhimu,vilabu vya Simba na Yanga vimepata afueni baada ya kufanikiwa kukamilisha taratibu zote za usajili za nyota wao wa kigeni ikiwemo kupata hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).
Simba ambayo leo itakuwa Mkwakwani Tanga kuivaa African Sports imefanikiwa kumaliza utata juu ya mlinzi wake wa pembeni Mrundi Emery Nimubona baada ya kuipata hati yake ya uhamisho na leo atakuwa dimbani jijini Tanga.
Upande wa pili nako Yanga inatarajiwa kuwatumia katika mchezo wake wa jumapili dhidi ya Coastal Union nyota wake wa kigeni toka Zimbabwe Thabani Kamusoko na Donald Ngoma baada ya kukamilika kwa uhamisho wao kutoka FC Platinum.
Awali kulikuwa na shaka kuwa nyota hao wasingeshuka dimbani baada ya kuwa hawajakamilisha taratibu stahiki za uhamisho wa kimataifa lakini sasa mambo yao yako safi.
0 comments:
Post a Comment