728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA SOKA TOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI MEI 8

    Graziano Pelle

    Sturridge Arsenal imeandaa kitita cha £30m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge.Sturridge,26 ameifungia Liverpool mabao 12 katika michezo 23. (Sunday Mirror)

    Giggs:Kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs amedaiwa kuwa ataachana na klabu hiyo ikiwa Jose Mourinho atapewa kibarua cha kumridhi Louis Van Gaal na yeye kutoswa.

    Keane:Vilabu vya Everton na Stoke City vimeripotiwa kuwa Katika mchuano mkali wa kuiwania saini mlinzi wa Burnley Michael Keane.(Sunday
    Mirror)

    Fabregas:Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas amekataa kujiunga na klabu moja ya China iliyotaka kumpa mshabara wa £200,000 kwa wiki baada ya kukatwa kodi.(The Sun on Sunday)

    Holding:Arsenal imepeleka ofa ya £10m kwenda Bolton kwa ajili ya kumsajili mlinzi Rob Holding,20. (Football Insider)

     Rodgers: West Brom itamgukia kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers ikiwa kocha wake wa sasa Tony Pulis atatimka klabuni hapo.

    Flores:Everton itamchukua kocha wa Watford Quique Sanchez Flores ili kuziba nafasi ya Roberto Martinez anayetarajiwa kufutwa kazi muda wowote kuanzia sasa.

    Pelle:Kocha mpya wa Chelsea Muitaliano Antonio Conte ameripotiwa kuwa atatoa kitita cha £8m ili kumsajili mshambuliaji asiye na furaha katika klabu ya Southampton Muitaliano Graziano Pelle,30.(Sun on Sunday)

    Deeney:Leicester City imepanga kutenga kitita cha £40m ili kuwasajili Yannick Bolasie wa Crystal Palace na Troy Deeney wa Watford (Sun on Sunday)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA SOKA TOKA BARANI ULAYA LEO JUMAPILI MEI 8 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top