728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 08, 2016

    YANGA BINGWA LIGI KUU BARA HII NI BAADA YA SIMBA KUCHAPWA 1-0 NA MWADUI

    Dar es salaam,Tanzania.

    YANGA SC imetwaa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hii ni baada ya Simba SC kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.

    Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 73 na Jamal Simba Mnyate.Mnyate alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ya Kevin Sabato aliyeunasa mpira mrefu uliopigwa na mlinda mlango Jackson Abdulrahman.

    Hii ina maana kwamba rasmi Yanga SC imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara kwani kati ya Azam FC na Simba SC hakuwa timu yenye uwezo wa kufikia pointi zake 68 walizonazo wana Jangwani hao.

    Katika mchezo mwingine uliopigwa huko Shinyanga CCM Kambarage Azam FC imeichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-1.

    Katika uwanja wa Sokoine huko Mbeya,wenyeji Tanzania Prisons imeichapa Majimaji kwa mabao 2-1 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA BINGWA LIGI KUU BARA HII NI BAADA YA SIMBA KUCHAPWA 1-0 NA MWADUI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top