Paris,Ufaransa.
MABAO mawili ya mshambuliaji Msweden Zlatan Ibrahimovic yameifanya Paris Saint-Germain imalize msimu wa 2015/16 kwa staili ya aina yake baada ya Jumamosi usiku kuichapa Marseille kwa mabao 4-2 na kutwaa taji la Coupe de France katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Stade de France jijini Paris.
Paris Saint-Germain ilianza kuandika bao la kuongoza mapema tu dakika ya 3 ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Blaise Matuidi kabla ya Marseille kusawazisha dakika ya 12 kupitia kwa winga wake Florian Thauvin na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili Paris Saint-Germain ilikuja kwa kasi na nguvu zaidi na kufanikiwa kupata mabao matatu ya kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic aliyefunga mabao mawili dakika za 47 na 82 na kufikisha mabao 50 msimu huu kabla ya kutengeneza jingine lililotiwa kimiani na Edinson Cavani dakika ya 57.
Dakika ya 87 mshambuliaji Mbelgiji Michy Batishuayi aliifungia Marseille bao na kufanya mchezo umalizike kwa Paris Saint-Germain kupata ushindi wa mabao 4-2 na kutwaa taji la Coupe de France ambalo ni la kumi katika historia.
Mataji mengine yaliyotwaliwa msimu huu na klabu hiyo yenye makao yake makuu jijini Paris ni Ligue 1 na Coupe de la Ligue.Hii ni mara ya pili kwa Paris Saint-Germain kumaliza msimu ikiwa na mataji matatu kibindoni mara ya kwanza ilikuwa ni msimu wa 2014/2015.
VIKOSI
Marseille (4-4-2): Mandanda; Manquillo,
N'Koulou, Rekik, Mendy; Isla, Barrada, Diarra,Thauvin; Batshuayi,Fletcher.
Akiba: Pele, Rolando, Dje Djedje,Romao, Alessandrini, N'Koudou, Cabella.
PSG (4-3-3): Sirigu; Aurier, Thiago Silva,Marquinhos, Maxwell; Stambouli, Matuidi,Rabiot; Di Maria, Ibrahimovic, Cavani.
Akiba: Douchez, Kurzawa, Van der Wiel,Luiz, Rimane, Lucas, Augustin.
0 comments:
Post a Comment