London,England.
Bao la dakika ya 110 la Kinda Jesse Lingard limeipa Manchester United ubingwa
wa 12 wa Kombe la FA na kuwa sawa na Arsenal baada ya jioni kuilaza Crystal Palace kwa mabao 2-1
katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa katika dimba la Wembley jijini London.
Crystal Palace ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika
ya 78 ya kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wake Jason Puncheon.Puncheon
alifunga bao hilo hilo akimalizia pasi nzuri ya mlinzi wa kulia Joel Ward.Hata
hivyo bao hilo halikudumu sana kwani dakika tatu baadae yaani dakika ya 81 Juan
Mata aliifungia Manchester United bao la kusawazisha baada ya kupokea pasi ya
kifua toka kwa Marouare Fellaini na kufanya matokeo kuwa 1-1hali iliyopelekea mwamuzi Mark
Clattenburg kuongeza dakika 30 ili kumpata mshindi.
Dakika ya 105 Manchester United ilijikuata ikibaki pungufu baada ya
mlinzi wake wa kati Chris Smalling kulimwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia
madhambi winga wa Crystal Palace Yannick Bolasie.Kadi hiyo nyekundu imemfanya
Smalling awe mchezaji wane kuwahi kukumbana na adhabu kama hiyo katika mchezo
wa fainali.Manchester United pia ilimpoteza Marcos Rashford aliyeumia.
Mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Louis Van Gaal ya kumtoa Juan Mata na
kumuingiza Jesse Lingard yalifanikiwa kuzaa matunda baada ya kinda huyo kufunga
bao la ushindi dakika ya 110 na kuisha Manchester United ifunge msimu na
kikombe hicho ambacho kwa misimu miwili mfululizo kilikuwa kikitwaliwa na
Arsenal.Huo ni ubingwa wa kwanza wa FA kwa Manchester United tangu mwaka 2004.
0 comments:
Post a Comment