London,England.
Meneja wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ametwaa tuzo ya meneja bora wa mwezi Octoba baada amewapiku mameneja Claudio Ranieli wa Leceister City na Manuel Pellegrini wa Manchester City.
Wenger ameitwaa tuzo hiyo baada ya kuiongoza Arsenal kushinda michezo minne kati ya minne ya ligi kuu England iliyopigwa katika mwezi Octoba.Katika kipindi hicho Arsenal ilifunga magoli 11 na kufungwa goli 1 pekee
Hii iankuwa ni tuzo ya pili ya mwezi kwa Arsenal Wenger ndani ya mwaka 2015 huku ikiwa ni tuzo ya 15 tangu aanze kuifundisha Arsenal miaka 20 iliyopita.Meneja anayeongoza kwa kutwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi ni Sir Alex Ferguson.
Kwa upande mwingine Jamie Vardy naye ameibuka kidedea baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Octoba.Vardy ametwaa tuzo hiyo baada ya kuifungia Leceister City magoli matano katika michezo minne ya ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment