London,England.
RONALDO hili ndilo jina la filamu ya gwiji wa soka duniani Cristiano Ronaldo iliyozinduliwa jana jumatatu huko Leceister Squire jijini London na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa soka.
Filamu hiyo ambayo imebeba historia ya kweli ya nyota huyo mzaliwa wa Madeira,Ureno inaelezea kila aina ya maisha na mikasa aliyopitia nyota huyo wa zamani wa Manchester United ikiwemo kifo cha baba yake mzazi kilichosababishwa na ulevi wa kupindukia.
Kisa kingine cha kusisimua katika filamu hiyo ni mama mzazi wa Ronaldo aitwaye Maria Dolores dos Santos Aveiro kukiri kuwa alitaka kuutoa ujauzito wa nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment