Paris,Ufaransa.
Winga wa Bayern Munich Mfaransa Frank Ribery amekiburuza mahakamani kituo cha runinga cha Marekani cha CNN baada ya kutumia picha yake bila ya makubaliano.
Ribery,32 amechukua hatua hiyo baada ya CNN kutumia picha yake katika habari ya mwanadada Chelsea Ake-Salvacion ambaye alikutwa amekufa katika tanki la mashine ya cryotherapy huko Nevada.
Octoba 28 kituo cha CNN kilirusha habari ya mwanadada huyo sambamba na picha ya Ribery akiwa katika mashine hiyo ambayo hutumiwa na wachezaji kuweka miili yao sawa.
Mwanasheria wa nyota huyo aitwaye Carlo Alberto Busa amesema mteja wake anataka alipwe dola milioni 1.5 kama fidia ya tukio hilo.
Picha iliyozua balaa
0 comments:
Post a Comment