728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 09, 2015

    DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO REAL SOCIEDAD

    Sociedad,Hispania.

    Klabu ya Real Sociedad imemtupia virago aliyekuwa kocha wake mkuu Mscotland David Moyes baada ya kudumu nae kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee.

    Real Sociedad "La Real" imefikia hatua hiyo baada ya Moyes (52) kushindwa kuinasua klabu hiyo toka mkiani mwa ligi ya La Liga kwani mpaka sasa miamba hiyo ya Hispania imefanikiwa kushinda michezo miwili tu kati ya michezo kumi na moja iliyocheza.Sociedad iko nafasi ya 16 ikiwa na pointi 9.

    Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Moyes kutupiwa virago katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja na nusu.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 katika klabu ya Manchester United.

    Mbali ya Moyes aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo Billy McKinlay nae pia ametupiwa virago.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO REAL SOCIEDAD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top