Geneva,Uswisi.
Shirikisho la soka duniani FIFA leo limetoa orodha mpya ya viwango vya soka.
Katika orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi,kwa mara ya kwanza UBELGIJI imepanda mpaka nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia pointi 1440 huku nafasi ya pili ikienda kwa Ujerumani iliyojikusanyia pointi 1338 nafasi ya tatu ikienda kwa Argentina iliyojikusanyia pointi 1383.
Kwa upande wa Afrika,Côte d'Ivoire (Ivory Coast) imerejea katika nafasi ya kwanza (Nafasi ya 22 Kidunia) na kuishusha Algeria (Nafasi ya 26 Kidunia) baada ya kujikusanyia pointi 890.Tanzania imepanda nafasi moja toka nafasi ya 136 mpaka 135.
TIMU ZILIZOKO KUMI BORA
1. Belgium 1440
2 Germany 1388
3 Argentina 1383
4 Portugal 1364
5 Chile 1288
6 Spain 1287
7 Colombia 1233
8 Brazil 1208
9 England 1179
10 Austria 1130
AFRIKA MASHARIKI
68 Uganda
96 Rwanda
107 Burundi
125 Kenya
128 Sudan
135 Tanzania
0 comments:
Post a Comment