Paris,Ufaransa.
Asubuhi ya jumatano ya leo imekuwa mbaya kwa straika Karim Benzema baada ya kushikiliwa na polisi kwa masaa kadhaa akifanyiwa mahojiano juu ya uwepo wa video ya ngono inayomuhusisha kiungo wa Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena.
Benzema alifika katika kituo hicho cha polisi kilichopo Versailles,Paris majira ya saa 9;00 asubuhi na kuanza kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za ulaghai juu ya uwepo wa video inayodaiwa kumuonyesha Valbuena akifanya mapenzi na binti mdogo.
Benzema ameingia hivi
Benzema amejikuta akiingia matatani baada ya mwanaume mmoja aitwaye Axel (39) ambaye alikuwa mtu wa karibu wa wakala wa klabu ya zamani ya Valbuena ya Marseille kudai kuwa ana video iliyorekodiwa kwa simu ikimuonyesha Valbuena akifanya mapenzi na binti mdogo na hivyo kumtumia ndugu wa karibu ili kumwambia Benzema amwambie Valbuena kuwa atoe €150,000 vinginevyo video hiyo ingerushwa You Tube na kwingineko.
Hoja inapojengwa
Baada ya Benzema kupata ujumbe ule aliamua kukaa chini na kumwambia Valbuena juu ya mkasa mzima na kumtaka kiungo huyo mfupi na machachari kutoa kiasi hicho cha pesa ili mambo hayo yaishe kitendo ambacho polisi inataka kujua kama kilikuwa ni kumlaghai ama kumsaidia Mathieu Valbuena.
Mpaka sasa watu watatu wako mikononi mwa polisi kutokana na kudaiwa kuwa nyuma ya tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment