728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 04, 2015

    YANGA YAMFUNGIA KAZI ELIAS MAGULI


    YANGA imewashusha presha mashabiki wake na kuwataka waache kuwa na mchecheto kwani benchi la ufundi la timu hiyo linajua kila kitu kinachohitajika kwenye kikosi cha timu yao katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na lazima wasajili straika mmoja wa maana kutoka hapa nchini.


    Habari ambazo DIMBA Jumatano limezipata na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, zinasema Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameanza kumfungia kazi straika wa zamani wa Simba anayekipiga Stand United, Elius Maguli wakitaka saini yake.



    Tangu kutua katika kikosi hicho cha Stand United akitokea Simba ambao walimuacha kwa madai ya kushuka kiwango, mshambuliaji huyo ni kama amefungwa mota kwenye miguu, kutokana na kazi anayoifanya uwanjani.



    Mpaka sasa straika huyo amefikisha mabao tisa akiwa kileleni mwa wafungaji akiwazidi akina Donald Ngoma wa Yanga mwenye mabao nane pamoja na Hamis Kiiza wa Simba mwenye idadi kama hiyo ya mabao.



    Straika huyo aliachwa na Simba baada ya kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mwingereza Dylan Kerr, kudai kuwa Maguli ambaye walimsajili kutoka kwa maafande wa Ruvu Shooting, hakuwa kwenye mipango yake.



    Kutemwa kwa Maguli katika staili hiyo ni kama kulimkera na kumuongezea hasira na sasa amekuwa akifunga kwa kadiri atakavyo huku akionyesha uwezo mkubwa ambapo hata yeye mwenyewe ameahidi kuzidi kuuwasha moto.



    Taarifa ambazo DIMBA Jumatano limezipata zinadai kuwa baadhi ya vigogo wa Yanga wanataka kufika bei ili kumchomoa Stand United aungane na akina Ngoma na Amissi Tambwe hasa katika kipindi hiki ambacho timu hiyo ikiwa kwenye harakati za kutetea ubingwa wake.



    Kwa habari kamili usikose kujipatia nakala yako ya Gazeti la DIMBA Leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAMFUNGIA KAZI ELIAS MAGULI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top