728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 04, 2015

    USAJILI DILISHA DOGO SIMBA WAVUJA


    SIMBA imesikia kiliocha mashabiki wake ambao wamekuwa wakiukosoa udhaifu uliopo kwenye kikosi chao na sasa uongozi wa timu hiyo umeamua kufanya kweli kwa kuleta mashine tatu hatari ambazo zitakuwa moto wa kuotea mbali.

    Ingawa uongozi wa Wekundu hao haujaweka wazi usajili huo uko vipi licha ya kupewa ripoti nzito na kocha wa timu hiyo Mwingereza, Dylan Kerr, lakini tayari siri hiyo imevuja na DIMBA Jumatano linaweza kukumwagia kila kitu baada ya kupenyezewa majina ya wachezaji wanaosajiliwa na wanaokatwa katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo.


    Mtoa habari wetu amelithibitishia DIMBA pasipo shaka kwamba, katika ripoti yake kocha Kerr, amebaini mapungufu katika safu ya ushambuliaji na kiungo, hivyo ameomba aletewe wachezaji watatu wa kigeni ambao wote ni ‘majembe.’


    Chanzo chetu kimesema kuwa Kerr amewaambia viongozi kwamba anataka straika mkali mwenye uwezo wa kufunga mabao kwa staili zote ambaye atasaidiana na Hamis Kiiza katika suala zima la kucheka na nyavu.

    Pia amewadokeza kwamba, anataka mshambuliaji mwingine ambaye kuna uwezekano mkubwa akahatarisha ajira ya Msenegal, Pape N’daw ambaye hana namba kwenye kikosi cha kwanza.


    Chanzo chetu kimesema Kerr amewaonyesha viongozi mastraika wawili ambao amewakubali baada ya kuelezwa juu ya wasifu wao na pia kuangalia mikanda yao ambapo kutoka nchini Uganda amewaambia anamtaka kiungo wa zamani wa Azam FC, Brian Majwega, huku pia akisisitiza kurejeshwa kwa Mkenya, Paul Kiongera ambaye anakipiga kwa mkopo katika klabu ya KCB ya Kenya.

    Habari zinasema kwamba, Kerr alimkubali Majwega tangu alipoonyeshwa mkanda wa video yake alipokuwa akichezea Azam na timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes,’ huku pia akivutiwa na nidhamu ya uchezaji ya Kiongera.
    Kwa habari kamili usikose kujipatia nakala yako ya Gazeti la DIMBA Leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI DILISHA DOGO SIMBA WAVUJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top