Paris,Ufaransa.
Kama unadhani kuwa Roman Abramovic ana mpango wa kumfuta kazi kocha Jose Mourinho andika umeumia.
Taarifa kutoa Ufaransa ambazo zimenaswa na gazeti la Daily Mail la Uingereza zinasema mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovic amekataa ofa ya paundi milioni 35 toka AS Monaco kwa ajili ya kumchukua Jose Mourinho.
Taarifa hiyo imemnukuu mmiliki mwenza wa AS Monaco Muitaliano Alessandro Proto ambaye mapema wiki iliyopita alikutana na Abramovic katika mitaani ya London na kumgusia mpango wa klabu yake kumtaka Mreno Jose Mourinho ambaye ana mkataba na Chelsea mpaka 2019.
0 comments:
Post a Comment