Ibe akipongezwa na kocha Klopp
Liverpool,England.
Liverpool imeendelea kuwa katika kiwango bora baada ya hapo jana usiku kuilaza Rubin Kazan kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa kundi B wa ligi ndogo ya Ulaya (Europa Ligi) uliopigwa huko Kazan Arena,Urusi.
Liverpool ambayo ilikuwa haijapata ushindi ugenini katika michuano ya Ulaya kwa kipindi cha miaka mitatu tangu ilipoishinda Udinese mwaka 2012 ilipata goli lake dakika ya 52 kupitia kwa kinda Jordan Ibe aliyemalizia kazi nzuri ya kiungo Mbrazil Arberto Firmino.
Kufuatia ushindi huo Liverpool imejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga katika hatua ya 32 bora ambapo ushindi dhidi ya Bordeaux wiki mbili zijazo utatosha kuipeleka miamba hiyo ya Anfield katika hatua hiyo muhimu.
Kwingineko Tottenham Hotspurs imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane baada ya kuilaza Anderletch kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa kundi J.Magoli ya Tottenham yamefungwa na Harry Kane dakika ya 29 na Mousa Dembele dakika ya 87 huku lile la wageni Anderletch likifungwa dakika ya 73 na Mnigeria Imoh Ezekiel.
Vilabu vilivyofuzu 32 bora mpaka sasa ni
Borussia Dortmund, Napoli, Molde na Rapid Vienna
Matokeo ya michezo yote ya Europa Ligi yako kama ifuatavyo.....
Ajax 0-0 Fenerbahçe
Celtic 1-2 Molde
FC Sion 1-1 Bordeaux
Rubin Kazan 0-1 Liverpool
Bor Dortmd 4-0 FK Qabala
FK Krasnodar 2-1 PAOK Salonika
Club Brugge 1-0 Legia Warsaw
Napoli 5-0 FC Midtjylland
Dinamo Minsk 1-2 Villarreal
Viktoria Plzen 1-2 Rapid Vienna
FC Groningen 0-1 Slovan Liberec
Marseille 1-0 Sporting Braga
Rosenborg 0-2 Lazio
St Etienne 3-0 Dnipro D'trovsk
Besiktas 1-1 L'motiv Moscow
S'kbeu Korce 3-0 Sporting
Belenenses 0-2 FC Basel
Lech Poznan 0-2 Fiorentina
FK Qarabag 1-1 Monaco
Tottenham 2-1 Anderlecht
Asteras Tripolis 2-0 Apoel Nic
Sparta Prague 1-1 Schalke
Ath Bilbao 5-1 P'zan Belgrade
FC Augsburg 4-1 AZ Alkmaar
0 comments:
Post a Comment