Andrey Coutinho
Dar es Salaam. Dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15 itashuhudiwa klabu mbalimbali za Ligi Kuu zikifanya mabadiliko kwenye vikosi vyao.
Yanga imepanga kumpiga bei kiungo wake mshambuliaji , Andrey Coutinho kwenye klabu ya St. George ya Ethiopia ambayo imekuwa ikionyesha nia ya kumtaka Mbrazili huyo.
Klabu hiyo imekuwa ikimhitaji mchezaji huyo raia wa Brazil kwa udi na uvumba kiasi cha kumtengea Dola 70,000 ili kunasa saini yake.Mapema mwaka huu, klabu hiyo ilituma maombi ya kumhitaji Coutinho, lakini mchezaji huyo aliikataa ofa hiyo.
Hata hivyo, Yanga imesema kwamba hakuna ofa yoyote ya maandishi ambayo imewasilishwa na St. George hadi sasa,hivyo inawawia vigumu kuzungumzia suala hilo.
0 comments:
Post a Comment