728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, November 10, 2015

    ARSENAL BHANA YAANZA KUHAHA KUMSAJILI TENA ILIYEMUUZA KWA BEI YA BAJAJ

    London,England.

    Arsenal kuna mambo,Arsene Wenger amekubali kula matapishi yake.

    Kutoka Daily Mail habari zinasema Arsenal inapambana na vilabu vya Westham United na Inter Milan kutaka kumsajili tena aliyewahi kuwa kiungo wake Oguzhan Ozyakup.

    Ozyakup,23 ambaye kwa sasa anakipiga na Besiktas ya nyumbani kwao Uturuki aliihama Arsenal mwaka 2012 kwa ada ndogo ya £350,000 baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

    Mpaka anaondoka Arsenal Ozyakup alikuwa amefanikiwa kuichezea klabu hiyo ya London michezo miwili tu tena yote ikiwa ya kombe la ligi (Carling Cup/Capital One).

    Kwanini Arsenal inamtaka tena??

    Tangu atue Beskitas,Oguzhan Ozyakup amekuwa ni moto wa kuotea mbali kwani mpaka tarehe ya leo kiungo huyo fundi amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 10 na kupika mengine 30.

    Habari za kuaminika ambazo pia zimeripotiwa na gazeti la Uturuki la AMK zinasema maafisa wa Arsenal walikuwa jijini Istanbul kumtazama nyota huyo ambaye goli lake la dakika za mwisho liliizamisha Bursaspor.

    Bei yake:Beskitas imeripotiwa kuwa tayari kumuuza Oguzhan Ozyakup ikiwa moja kati ya vilabu vinavyomtaka vitakuwa tayari kutoa ada ya £8m.










    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL BHANA YAANZA KUHAHA KUMSAJILI TENA ILIYEMUUZA KWA BEI YA BAJAJ Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top