Dar es Salaam,Tanzania.
KAMPUNI ya kutengeneza vifaa vya michezo ya MACRON TECHNICAL SPORTS WEAR yenye makao yake makuu nchini Italia imevutiwa na klabu ya Yanga SC hivyo iko tayari kufanya nayo biashara/kuidhamini.
Macron imefikia hatua hiyo baada ya kuvutiwa na mafanikio ambayo Yanga SC imeyapata siku za hivi karibuni hasa katika mashindano ya kimataifa.
Kwa kuanzia Macron itaivisha Yanga SC jezi zake mpya katika mchezo wake wa kwanza wa kombe la shirikisho dhidi ya MO Bejaia unaotarajiwa kuchezwa Juni 19 huko Bejaia nchini Algeria.
Ikiwa Yanga SC itavutiwa na jezi hizo toka Macron,pande hizo mbili zitakaa mezani na kuangalia uwezekano wa kufanya kazi pamoja.
Tayari Kampuni hiyo kwa Afrika imeshaanza kufanya kazi na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Misri klabu ya Zamalek.
Hongera Yanga
ReplyDelete