Kwa mara
nyingine mshambuliaji mtata Mario Balotelli amejikuta akitupwa nje ya kikosi
cha timu ya taifa ya Italia na kocha mpya Antonio Conte huku mshambuliaji wa
Southampton Graziano Pelle akiitwa kwa mara ya kwanza baada ya kuendelea
kuonyesha kiwango kizuri tangu atue England.
Pelle ambaye
msimu uliopita aliifungia klabu yake ya zamani ya Feyenoord ya Uholanzi magoli
23 katika michezo 28 tayari ameshatikisa nyazu za timu pinzani za Epl mara 4
katika mechi 6 tu.
Balotelli
ambaye tangu atue Liverpool ameshinda kuwika kiasi cha kuanza kuwatia shaka
baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo ya Merseyside,hii imekuwa ni mara yake ya
pili kutemwa na kocha huyo mwenye msimamo mkali na mwenye kuzingatia nidhamu
nje na ndani ya uwanja.
Mbali ya Balotelli
nyota wengine waliotemwa
katika kikosi kitakachoivaa Azerbaijan ijumaaa na Malta siku tatu baadae ni pamoja na wakongwe Andrea Pirlo pamoja na Daniele De Rossi.
katika kikosi kitakachoivaa Azerbaijan ijumaaa na Malta siku tatu baadae ni pamoja na wakongwe Andrea Pirlo pamoja na Daniele De Rossi.
Kikosi
kamili kiko kama ifuatavyo……..
Makipa: Gianluigi Buffon (Juventus), Mattia Perin (Genoa), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain).
Walinzi:
Leonardo Bonucci (Juventus), Giorgio Chiellini (Juventus), Angelo
Ogbonna (Juventus), Andrea Ranocchia (Inter Milan), Daniele Rugani
(Empoli).
Viungo: Alberto Aquilani (Fiorentina), Giacomo Bonaventura (Milan), Antonio
Candreva (Lazio), Matteo Darmian (Torino), Mattia De Sciglio (AC Milan),
Alessandro Florenzi (Roma), Claudio Marchisio (Juventus), Marco Parolo
(Lazio), Manuel Pasqual (Fiorentina), Andrea Poli (Milan), Thiago Motta
(Paris Saint-Germain), Marco Verratti (Paris Saint-Germain).
Washambuliaji: Mattia Destro (Roma), Sebastian Giovinco (Juventus), Ciro Immobile
(Borussia Dortmund), Pablo Osvaldo (Inter Milan), Graziano Pelle
(Southampton), Simone Zaza (Sassuolo).
0 comments:
Post a Comment