HALI ya mambo inaonekana siyo shwari baina ya timu
mbili kutoka mkoani Mbeya na Tanga, ambapo imani za kishirikina
zimetajwa kuhusika na sasa kila upande umeamua kukimbilia kushitaki kwa
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).
Coastal Union walifungwa bao 1-0 na Mbeya City kwenye Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya, lakini baada ya mchezo huo Coastal wakaibuka na
kusema wenyeji wao hao waliwafanyia vitendo vingi vinavyohusiana na
imani za kishirikina, Mbeya City kusikia hivyo, wakakanusha vikali na
kusema hawako
tayari kudhalilishwa.
Kiongozi wa msafara na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal,
Albert Clement Peter, ameliambia gazeti hili kuwa vitendo walivyofanyiwa
na Mbeya City havikuwa vya kiuungwana hata kidogo hivyo wamepeleka
barua yao TFF.
“Walianza kufanyiwa usiku katika hoteli tuliyofikia ya…(anaitaja),
hata chumba cha kubadilishia nguo uwanjani kilipigwa rangi na
tukashindwa kuingia. Tumeshapeleka barua ya kushitaki TFF,” alisema
Albert.
Upande wa Mbeya City kupitia Ofisa Habari, Dismas Ten alisema kipigo
kiliwachanganya wapinzani wao na ndiyo maana wanaanza kusingizia masuala
ya ushirikina jambo ambalo si la kweli.“Suala hili tutalipeleka TFF,
hicho wanachokisema ni udhalilishaji wa wazi,” alisema Ten.
Habari kwa msaada wa Global publishers
0 comments:
Post a Comment