Nilipata fursa ya kutizama mechi ya Taifa Stars dhidi ya Benin. Ndio ilipendeza kweli, kila mchezaii alitekeleza majukumu ipasavyo, timu ilicheza kwa uwiiano murua, mfumo mpya ambao nilihisi ungetusumbua nao ulifanikiwa haswa, mwisho nikageukia ubao wa matokeo, Taifa Stars iikuwa ikiongoza bao 4 kwa 1. Hata Benin nao walishakata tamaa, hawakuweza kufungua kufuli za Taifa Stars. Ilibidi tu nifanye kutizama mashabiki walikuwa na hisia gani, wote walishangilia sana, ikabidi nisikilize mahojiano ya naodha wa timu ya Taifa, nao vile vile aliyehoji na aliyehojiwa wote walibeba maswali na majibu yenye furaha tupu. Nikageukia tena upande wa mashabiki nione hata kama kuna mmoja aliyefikiri ama kuwaza kama mimi, sikumuona wengi walikuwa wameweka viganja shingoni kuashiria ile namna maarufu ya ushangiliaji maarufu sana CHINJA.
Nikatoa simu mfukoni kumpigia Rafiki yangu ambaye baada ya Msumbiji kisha Burundi alinambia Timu ya Taifa isimamishwe tuwekeze kwenye kilimo kwanza naye akapokea kwa kicheko sana ananiuliza umemuona KIEMBA? Nikajua 80%kama sio Zaidi ya Watanzania walifurahishwa na matokeo hayo, hata wale walioshaanza kupoteza Imani, nikamkumbuka mwalimu wangu mmoja wa URAIA, aliwahi kunambia “A SHORT TIME HAPPINESS CAN CHANGE THE WHOLE HUMAN’S THOUGHTS, THAT’S IT HAPPINESS IS BLINDNESS” alimaanisha “FURAHA YA MUDA MFUPI INAWEZA BADILI MFUMO MZIMA WA MAWAZO YAMWANADAMU, NDIO HIVYO FURAHA NI UPOFU”.
Sikutaka kuamini moja kwa moja mpaka niwasikilize wachambuzi na wahandishi wa michezo, nao waliandika kilekile na kusema kilekile nikakubaliana na mwalimu wangu kabisa. Hakuna aliyekumbuka tena Taifa Stars inaelekea wapi kwa Muda huo.
Wakati natizama goli bora la siku la Kiemba, nilishuhudia pasi kutoka kwa Mwinyi kisha kwa Ngasa ingawa haikumfikia ikapokelewa na Kiemba baada ya beki kujaribu kuokoa, nikaita goli liliokula chumvi, yaani limepita kwa watu wenye ndevu, lakini wakati nawaza hayo ikabidi nistuke nikatizama waliokuwa wanamlinda Kipa, walikuwa ni Nadir, Oscar, Nyoni, Kapombe na Morris, kisha nikamtizama na kipa mwenyewe hakuwa Aishi Manura au Casillas ingawa Dida alikuwa benchi. Hapo ndipo akili yangu ikawaza tofauti na wengine wengi, akili yangu ikawaza miaka ya mbele kidogo, akili yangu ikawaza 2017 na 2018.
Ndio katika kikosi kilichotoa burudani nzuri wenye uhakika wa kuwepo miaka hiyo ni watatu tu, Chanongo, Ulimwengu na Kapombe kidogo na Ngasa kama akijua kuitumia kasi na kuutunza mwili wake vyema. Maana ake wachezaji muhimu Zaidi katika ushindi dhidi ya Benin Zaidi ya Nusu tumekaribia kuwapokea jukwaani kama Taifa Stars ikiwa inacheza. Hapa ndipo nikawaza, je tunaliona hili? Tunaiwaza 2017 kweli AFCON maana nasikia tumetemwa uandaaji? Au tunaitamani Urusi kombe la dunia? Sitaki kuubeza ushindi wetu dhidi y Benin ila swali ni je tumetumia njia sahihi kwa maandalizi ya miaka hiyo? Tuna miaka mitatu ya kufika pale bahati mbaya ya Watanzania ama Waafrica tunapaona mbali, maana tunajiuliza siku 1065 si haba, hapa ndipo mawazo yetu yalipo kwa sasa, tunalishangilia goli la Kiemba kwa Nguvu huku tukiamini siku bado tunazo.
Aliyewahi kuwa Rais wa Marekani ABRAHAM LINCOLN aliwahi kusema kuwa “GIVE ME 6 HOURS TO CHOP DOWN THE TREE AND I’LL SPEND FOUR SHARPENING AN AXE” Alimaanisha kama ukimpa masaa sita kuangusha mti basi yeye atatumia masaa manne kati ya hao akinoa shoka yake. Alitambua analolisema, maandalizi uifanya kazi kuwa rahisi Zaidi, ukupa uhakika Zaidi na ukuongezea ufanisi Zaidi. Hapa ndipo tumefeli watanzania, tunaona muda tunao wa kupigana na mti wakati shoka likiwa butu, tunafurahi matawi yakidondoka(Benin) na kulisahau shina linatungoja(AFCON na KOMBE LA DUNIA). Hata Bruce Lee mpiganaji karate wa zamani leo marehemu aliwahi kukiri kuwa “NAMUOGOPA MTU ANAYEJIFUNZA TEKE MOJA MARA 10,000 LAKINI SIWEZI MUOGOPA ANAYEJIFUNZA MATEKE 10,000 MARA MOJA”. Alimaanisha jambo jepesi tu ufanisi, huwezi kuwa fanisi kama wewe ni mtu wa majaribio kila kukicha, miaka tuliyowahitaji Zaidi akina Kiemba nafasi zao walicheza akina Maulidi, Miaka ya kina Ngasa walicheza akina Boban na leo miaka ya maandalizi ya kina Msuva, Aishi, tunamkimbilia Kazimoto. Tunafarijika sana na kiwango chake, tunacheka kisha tunapita pale Rose Garden Kijitonyama tunafungua vinywaji na kuwaza namna ya kuwatuza, tunaanza kuwaza na namna ya kumrejesha Kiemba kikosi cha kwanza katika klabu yake ya Simba, baadae msimu mpya tunamtambulisha Kazimoto jangwani na kumlipa pensheni ya milioni 5 kwa mwezi, kisha maisha yanasona na Msuva anarejea benchi.
Nilikuwa natamani nami nijiunge katika wimbi la furaha lakini nafsi inanisuta, nafsi inanieleza mwaka 2018 wakati Taifa Stars ikicheza mechi ya kirafiki na Tahiti maana itakuwa ndio kipimo chetu wakati huo nani anajua,nitakuwa jukwaani natizama mechi pamoja na Cannavaro, Kiemba, Morris, Mwadini, Kazimoto, Yondani pengine na Ngasa na kwa nyakati tofauti watanieleza Nicasius hii timu inahitaji vijana wapandeili tushiriki pale Qatar 2022, hawa akina Ulimwengu waanze kupumzishwa, na si haba watakua wamesahau kuwa Taifa lilishangilia mabao yao dhidi ya Benin na kutupofusha maisha ya miaka hiyo watakayokuwepo jukwaani. Ulipata kumfahamu CLIVE STAPLES LEWIS? Mwandishi maarufu wa vitabu Uingereza, aliwahi kusema “THE HUMAN MIND IS GENERALLY FAR MORE EAGER TO PRAISE AND DISPRAISE THAN TO DESCRIBE AND DEFINE” alimaanisha kwa kawaida akili ya mwanadamu huwa na hamu ya kusifia ama kutokusifia kuliko kufafanua na kuelezea. Pengine hii nayo inatutafuna, kila nikitazama mataifa yaliyoendelea kisoka naona huu ndio muda vijana wanapewa nafasi kuandaa kwa ajili ya hayo mashindano hata Cameroon hawana Eto’o, Ivory Coast hawana tena Drogba na akina Zokora, ila sie tunao wengi. Hata uingereza wenye tabia kama zetu za Ugonjwa wa Clive Lewis nao wameacha hili, Hispania pia, Ujerumani waigundua mapema. Nasubiri kwa hamu kukaa Jukwaani na Kiemba 2018, lakini majibu ya maswali yake au hoja zake tayari ninayo, hata yule Rafiki angu najua atanipigia tena simu kama sio yeye basi mwingine, wakati Benin akiwa World Cup kipindi hicho ataniuliza umeona goli la SAMATA dhidi ya TAHITI?,ntamjibu FURAHA NI UPOFU, najua hatowaza Qatar, Kiemba nae FURAHA NI UPOFU hatukuwaza URUSI, naamini tutakaa jukwaa moja. Ahsante mwalimu wangu hata sisi wahandishi wengi tumepofuliwa na Furaha ya bao la Kiemba. Ahsanteni
Nicasius Coutinho Suso
Email: nnicasius@outlook.com
Mobile: 0712203770
0 comments:
Post a Comment