Kitimtim cha ligi kuu ya England kitaendelea
tena kesho wakati ambapo mashabiki wa soka
nchini humo na duniani kote watapata nafasi
ya kuzishuhudia timu zao zikitafuta pointi tatu
muhimu.
Newcastle Utd wataikaribisha Liverpool katika
mchezo ambao utarushwa moja kwa moja
kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC majira ya
saa tisa unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Arsenal wao wataikaribisha Burnley, huku
Chelsea nayo wakiialika QPR. Everton
watakuwa nyumbani kucheza Swansea City.
Hull City wataikabili Southampton. Michezo
mingine ni itakayochezwa siku hiyo ya kesho
ni kati ya Leicester City watakapo kwaana na
West Brom, Huku Stoke City watakapoikabili
West Ham utd.
Siku ya jumapili ni mpambano wa kukata na
shoka ambapo Manchester United
wataavaana na Manchester City mechi
ambayo pia itatangazwa moja kwa moja na
Idhaa ya Kiswahili ya BBC ,huku Tottenham
watakapokwaana na Aston villa.
0 comments:
Post a Comment