Mshambuliaji
wa klabu ya Real Madrid Mfaransa Karim Benzema anaamini kuwa lazima klabu ya
Barcelona ibaki La Liga hata kama jimbo la Catalunya inakotoka klabu hiyo litafanikiwa
kutimiza ndoto yake ya kutaka kujitenga na Hispania na kuwa taifa
linalojitegemea.
Wakati
mbichi na mbivu za sakata hilo lililodumu kwa kipindi kirefu sasa likisubiri
Novemba 22 mwaka huu kujua kama Catalunya itaachiwa na kuwa taifa huru tayari
raisi wa chama cha soka cha Hispania (LFP) Javier Tebas ameshatanabaisha kuwa
mabingwa hao wa mara 22 wa taji la La Liga na wapinzani wao wa mji mmoja klabu
ya Espanyol hawataruhusiwa
kushiriki tena ligi hiyo mara jimbo hilo
litakapokuwa limejitenga.
Lakini
Benzema anahisi kuwa ni muhimu Barcelona
ikaendelea kuwepo La Liga amesema
“Tunaihitaji Barcelona ibaki kwenye
ligi.Hakuna kitu kikubwa kama kuiona Barcelona ikiumana na Madrid”
“Kama wanataka kujiondoa La Liga hilo
litakuwa ni tatizo,napenda mambo yabaki kama yalivyo na Barcelona tuendelee
kuwa nao”Alimaliza
Benzema
Taarifa zilizoibuka
jana zinasema kuwa tayari maafisa wa klabu ya Barcelona wameshaanza kufanya
mpango wa kuihamishia klabu hiyo katika ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1
kama hawatotambuliwa baada ya jimbo lao kujitenga.
0 comments:
Post a Comment