Mshambuliaji
mkongwe wa klabu ya Roma ya Italia Francesco Totti licha ya kuisaidia klabu
yake kuondoka na pointi moja (1) dhidi ya klabu ya Manchester City katika dimba
la Etihad jijini Manchester usiku wa jana katika michuano ya ligi ya mabingwa
wa Ulaya pia aliweka rekodi
ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi
kufungwa goli katika michuano hiyo.
Totti ambaye
kwa sasa ana umri wa miaka 38 na siku 3 alifunga goli hilo dakika ya 23 ya
mchezo huo na kusawazisha goli la mapema la mshambulaji Sergio Aguero na
hatimaye kuvunja rekodi hiyo iliyokuwa ikishikiriwa na nyota wa zamani wa klabu
ya Manchester United Ryan Giggs aliyefunga akiwa na miaka 37 na siku 290 dhidi
ya klabu ya SL Benfica mwaka 2011/12.
Orodha
kamili ya nyota wenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga goli katika michuano ya
ligi ya mabingwa hii hapa…..
Francesco Totti – 38 years 3 days – Manchester City v AS Roma, 30/09/14
Ryan Giggs – 37 years 290 days – SL Benfica v Manchester United FC, 14/09/11
Filippo Inzaghi – 37 years 87 days – AS Milan v Real Madrid CF, 03/11/10
Javier Zanetti – 37 years 72 days – FC Internazionale Milano v Tottenham Hotspur FC, 20/10/10
Laurent Blanc – 36 years 339 days – Olympiacos FC v Manchester United FC, 23/10/02
Paolo Maldini – 36 years 334 days – Liverpool FC v AC Milan, 25/05/05
0 comments:
Post a Comment