Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Urusi Muitaliano Fabio Capello ameibuka na kusema nyota wa Barcelona Lionel Messi ni dhaidi ya mpinzani wake Cristian Ronaldo kwakuwa ana vitu ambavyo nyota wengine dunia hawana.
Capella akifanya mahojiano na gazeti la As la Urusi amesema Messi na Ronaldo ni wachezaji wa kipekee sana lakini kuna tofauti kubwa kati yao.
Amesema ``Namuheshimu sana Ronaldo,ni mchezaji mzuri sana na mwenye nguvu lakini hana ufundi wa asili kama alionao Messi.Messi ni mchezaji wa kipekee zaidi huwezi kumlinganisha na yeyote,hakabiki kirahisi."
Pia Capello amekiri kuwa alitaka kumsajili nyota huyo kwa mkopo mwaka 2005.
Anasema ``Ilikuwa ni katika mchezo wa kombe la Gamper kati ya timu yangu ya Juventus wakati huo na Barcelona ya Frank Rijkaard.Nilibaki mdomo wazi baada ya Messi kuipasua kama karatasi safu ngumu ya ulinzi ya Juventus ikiongozwa na Fabio Cannavaro.Baada ya tukio lile nikajikuta nataka kumsajili Messi kwa mkopo wakati mchezo ukiendelea jambo ambalo lilikuwa siyo kawaida"
``Wakati nikitafakari hilo mpira ulisimama nikamfuata Rijkaard na kumwambia humchezeshi Messi kwakuwa una nyota watatu wa kigeni katika kikosi chako sasa kwanini usinikopeshe kinda huyu kwa msimu mmoja?
Rijakaard akanijibu ``Tunafanyia kazi suala la kuhakikisha Messi anapata hadhi ya kucheza La Liga na hilo huenda likakamilika baada ya miezi mitatu au minne hivyo hatutokupa kwa mkopo atabaki kusubiri hapa hapa jambo hilo likamilike".
0 comments:
Post a Comment