728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 10, 2014

    IJUE TIMU YA TAIFA YA BENIN (Les Ecureuils)


    Tukiwa tunajiandaa na mchezo wa  kimataifa wa kirafiki kati ya timu yetu ya taifa (Taifa Stars)dhidi ya wageni timu ya taifa ya Benin maarufu kama Les Ecureuils katika dimba la uwanja wa taifa jumapili ya Octoba 12,pata kuijua timu hiyo japo kwa ufupi.

     
    Timu ya taifa ya Benin ama Les Ecureuils (The Squirrels) inasimamiwa na kuendeshwa na chama cha soka cha nchi hiyo kiitwacho “Federation Beninoise de Football” ambacho ni mwanachama wa FIFA,CAF na WAFU (Chama cha soka cha Africa Magharibi)
    .
    Timu hii ilikuwa ikijulikana kwa jina la Dahomey mpaka hapo mwaka 1975 ilipokuja kubadilishwa jina na kuitwa Benin.Benin  kama ilivyo kwa Tanzania haijawahi kushiriki fainali zozote zile na kombe la dunia tangu lilipoanzishwa mwaka 1930 huko Montevideo Uruguayi na kushuhudia wenyeji Uruguayi wakilibakiza kombe hilo nyumbani kwao.

     Benin imeshafanikiwa kushiriki michuano ya mataifa huru ya Africa (AFCON)  mara  tatu (3) ikiwa ni 2004,2008 na 2010.Mpaka sasa Benin imeshapitia mikononi mwa makocha 15 baadhi yao ni Wabi Gomez,Peter Schnittger (1992),Herve Revelli (2004),Manuel Amoros (2012-2014) na sasa Didier Olle Nicolle (2014-)

    REKODI MBALIMBALI
    ·         Katika orodha ya ubora wa viwango vya soka kwa mujibu wa FIFA toleo la Septemba 18,2014) Benin iko nafasi ya 78 huku nafasi ya juu kabisa iliyowahi kufikia ni 59 (Novemba
    2009-April 2010)na julai 1996 ikishika nafasi ya 165.

    ·         Mchezo wake wa kwanza Benin wakati huo ikiitwa Dahomey  ilicheza na timu ya taifa ya Nigeria November 8,1959 na kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Dahomey na katika mchezo wa marudiano uliopigwa Lagos Novemba 28,Benin ililala kwa jumla ya goli 10-1.

    ·         Usindi mkubwa:Benin ilipata ushindi wake mkubwa  wa goli 7-0 Disemba 27,1961 dhidi ya Mauritania



      Mfungaji anayeongoza kwa kuifungia magoli Benin ni Razak Omotoyosi anayekipiga na klabu ya Kahramanmaraşspor  akiwa na magoli 21 huku nahodha wa timu hiyo akiwa ni Stephane Sessegnon anayekipiga na klabu ya West Bromwich Albion ya England.

    ·         Timu ya taifa ya Benin inatumia uwanja wa Stade de I’Amitie kwa mechi zake za nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IJUE TIMU YA TAIFA YA BENIN (Les Ecureuils) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top