Ukitazama kwa makini katika benchi la klabu ya Chelsea utamwona
mwanamke mrembo sana,mikononi akiwa amevaa gloves raini na karibu yake
kukiwa na kisanduku kidogo bila shaka ni cha huduma ya kwanza akiwa
amekaa kimya nyuma ya kocha wa klabu hiyo mwenye maneno mengi Mreno Jose
Mourinho.Moja kwa moja unapata hamu ya kutaka kujua japo mambo machache
kumuhusu.
Mrembo huyo anaitwa Eva Carneiro ni dakatari wa klabu hiyo ambapo yeye na mwenzake akina Stuart Sullivan,Kate Jordan na Jason Palmer jukumu lao kubwa ni kuhakikisha afya za wachezaji wa klabu ya hiyo zinakuwa salama muda wote ndani na nje ya uwanja kwa tiba bora na ushauri.
Eva alizaliwa huko katika visiwa vya Gibraltar vinavyomilikiwa na Uingereza toka kwa baba Muhispania na mama Muingereza.Alipata elimu yake ya udaktari wa michezo na mambo mengine katika chuo kikuu cha Nottingham na kufanikiwa kufanya kazi za kujitolea katika nchi za Scotland na Australia kabla ya kurudi tena London na kujiunga na chuo Kikuyu cha Queen Mary na kupata bahati ya kuongeza ujuzi na uzoefu zaidi katika klabu ya West ham.
Je,ni lini alijiunga na klabu ya Chelsea?
Baada ya kufanya kazi na taasisi ya British Olympic Medical Institute kama daktari wa timu ya taifa ya riadha ya England iliyoshiri michuano ya Olympic huko Beijing,China mwaka 2008 na kwa nyakati fulani akitumika katika timu ya soka ya wanawake ya nchi hiyo Eva alijiunga rasmi na klabu ya Chelsea mwaka 2009 kama daktari wa kikosi cha wachezaji wa akiba.
Lini alianza kuupenda mchezo wa soka?
Kama mwaka 1998 kusingekuwa na michuano ya kombe la dunia pale Ufaransa basi mapenzi ya Eva katika mchezo huu yangeanzia mwaka 2002 katika michuano mingine ya kombe hilo pale Korea na Japan.
Eva anasema ``Nilianza kuupenda mchezo wa soka mwaka 1998.Nakumbuka ilikuwa ni katika mchezo wa kombe la dunia kati ya Ufaransa ya Zidane dhidi ya Mexico ya Branco.Nikiwa katika chumba cha hoteli moja niliyofikia mjini Mexico City,sikuwa na kitu cha kufanya jioni ile baada ya kumaliza shughuri zangu zote mchana nikajikuta nakaa na kuanza kutazama mchezo ule na hapo ndipo nilipojikuta navutiwa.
Je,baada ya kurudi England akitokea Mexico alifanya nini?
Alianza kucheza soka lakini baada ya muda mfupi aliacha kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Anasema ``Niliumia mara nyingi nikaamua kuacha kucheza.Akili yangu nikaikita katika fani ya udaktari wa masuala ya michezo ili kusaidia wanamichezo kupambana na majeraha pindi wawapo viwanjani kutimiza majukumu yao ya kila siku.
Je,Eva ni shabiki wa Chelsea pia ama kuna klabu nyingine anayoishabikia?
Kabla hajakujibu swali hilo kwanza atatabasamu,ataangalia kushoto na kulia kujua kama hakuna mtu yeyote anayemuangalia kisha atakujibu kwa kukunong'oneza Real Madridddddd!!Ndiyo!!Eva ni shabiki wa Real Madrid na hilo ameshindwa kulificha kama afanyavyo katika mambo yake mengine.Ukitaka ujue kama atalia ama atacheka ombea timu hizo zikutane katika ligi ya mabingwa tena katika hatua ya mtoano.
Je, kipi kimeshawahi kumliza na kumuumiza moyo sana tangu atue klabuni hapo? Bila shaka atakujibu kufukuzwa kwa Andres Villas Boaz toka katika nafasi yake ya ukocha.Boaz ndiye aliyempandisha daraja mrembo huyu toka kuwa daktari wa kikosi cha vijana kile cha akina Adam Nditi mpaka kikosi cha wakubwa cha akina Michael Essien naJohn Terry hiyo ikiwa ni mwaka 2011.
Je,nje ya uwanja furaha ya Eva huletwa na nini?
Viko vingi ila sana sana Eva hupendelea kusafiri safiri,kusikiliza muziki wa Salsa,Samba hupendelea pia michezo ya kuteleza majini maarufu kama surfing.
Je,ni kweli wachezaji wa Chelsea huwahiana kukaa karibu yake?
Kuna uvumi uliowahi kuvuma zamani kuwa baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo hufanya kila mbinu ili wapate kukaa karibu yake wakati wa mechi.Inasemekana Fernando Torres alipenda sana kukaa jirani na mrembo pengine kuliko hata kucheza ndiyo maana mpaka anatimkia Ac Milan kwa mkopo hakuwahi kusema anachukia kukaa benchi.
Je,Eva ana mume au mchumba?
Ana mchumba na ni mama wa mtoto moja wa kike
0 comments:
Post a Comment