728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 29, 2014

    ANCELOTTI NI NGUMU KUMNYAMAZISHA BLATTER

    Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti ameibuka na kusema ni ngumu kumziba mdomo raisi wa FIFA Sepp Blatter.

    Ancelotti ameyasema hayo baada ya mapema wiki hii raisi huyo kuibuka na kudai kuwa Lionel Messi alipewa kimakosa tuzo ya mchezaji bora katika fainali zilizopita za dunia nchini Brazil na badala yake tuzo hiyo ilipaswa iende kwa mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer.

    Kauli hiyo ya Blatter imetafsiriwa na wengi kuwa ni njama ya kumpigia kampeni kijanja Neuer badala ya Cristiano Ronaldo ambaye kwa macho ya wengi ndiye anayetazamwa kama mshindi.

    Ancelotti amesema ``Ni ngumu mno kumnyamazisha Blatter na mara nyingi nimekuwa nikishangazwa na maneno yake.Ila katika hili sidhani kama lina maana.Ronaldo amefanya makubwa ametwaa makombe muhimu kama Copa del rey na ligi ya mabingwa huku akiendelea kufunga magoli kila kukicha.Dunia nzima inajua tuzo hii tayari ina mwenyewe ambaye ni Ronaldo"

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ANCELOTTI NI NGUMU KUMNYAMAZISHA BLATTER Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top