Nyota wa klabu
ya Arsenal Alexis Sanchez amekiri kuwa anachukizwa mno na kitendo cha kuwekwa
benchi na kocha Arsene Wenger na kuongeza kuwa nafasi aipendayo ni wingi ya
kushoto.
Tangu atue
klabuni hapo tayari Sanchez ameshatumiwa katika nafasi zote za
ushambuliaji,wingi zote kulia na kushoto pamoja na ushambuliaji wa kati.Akifanya
mahojiano na tovuti ya klabu hiyo Sanchez mwenye magoli matano mpaka sasa
amekiri kukasirishwa kutolewa katika mchezo dhidi ya Galatasaray pamoja na
kuanzia benchi katika michezo miwili ya ligi dhidi ya Aston Villa na Tottenham.
Amesema
“Naweza kukimbia na kuingia
ndani vizuri nikitokea kushoto lakini nafasi yoyote ile ni nzuri kwangu ilimradi nacheza mpira kuliko kukaa benchi”
“Naweza kukimbia na kuingia
ndani vizuri nikitokea kushoto lakini nafasi yoyote ile ni nzuri kwangu ilimradi nacheza mpira kuliko kukaa benchi”
“Ukinitoa mchezoni ni sawa na
kuniibia mpira miguuni mwangu”
“Nataka kushinda kila kitu,ukitazama
aina ya kocha tuliyenaye,wachezaji waliopo na njaa waliyonayo,tunaweza kushinda
karibu kila kitu”
Wakati huo
huo nyota huyo amesema kuwa ligi ya England ni ngumu kuliko ile ya Hispania
lakini inavutia.
0 comments:
Post a Comment