Taarifa
kutoka ndani ya klabu ya Liverpool zinasema klabu hiyo iko mbioni kumnasa
kiungo wa klabu ya Newcastle Cheick Tiote kwa dau la paundi milioni 15.5 hapo
mwezi januari.
Liverpool
inaonekana kuipiku Arsenal na kukalia kiti cha uongozi wa mbio za kumnasa
kiungo huyo asiye na masihara pindi awapo dimbani.Tiote hivi karibuni ameiambia
klabu yake kuwa
muda wake wa kutafuta changamoto mpya umefika hivyo Newcastle iheshimu
maamuzi hayo.
Inasemekana
Newcastle inataka angalau kiasi cha paundi milioni 20 ili iweze kumuachia
kiungo huyo iliyemsajili miaka minne iliyopita toka klabu ya FC Twende ya Uholanzi.
0 comments:
Post a Comment