HII ni kali. Mashabiki wa Liverpool
wameripotiwa kurudisha jezi za Mario
Balotelli walizonunua baada ya staa huyo
kujiunga na timu hiyo ili wapewe za
mastaa wao makini baada ya Mtaliano
huyo kuchemsha.
Mashabiki kadhaa walionekana
wakipanga mstari na jezi zao zilizokuwa
zimeandika ‘Balotelli 45’ mgongoni kuvua
ili kupewa nyingine za mastraika
waliofanya vizuri kwenye kikosi hicho
kama Rush, Fowler na Owen.
Tukio hilo lilifanyika Jumamosi iliyopita
kwenye mechi dhidi ya Hull City baada ya
mashabiki hao kukerwa na kitendo cha
Balotelli kubadilishana jezi na Pepe wa
Real Madrid wakati wa mapumziko
kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
iliyomalizika kwa Liverpool kuchapwa
mabao 3-0.
0 comments:
Post a Comment