728x90 AdSpace

Tuesday, October 28, 2014

FLAMINI:SANCHEZ KAMA THIERRY HENRY

Kiungo wa klabu ya Arsenal Mfaransa Mathieu Flamini amemwagia sifa winga wa klabu hiyo Mchile Alexis Sanchez na kudai kuwa nyota huyo atapata mafanikio kama nyota wa zamani wa klabu hiyo Thierry Henry na Robin Van Persie.

Sanchez ambaye mpaka sasa ameifungia Arsenal jumla ya mabao manane katika michuano hiyo ameibuka na kuwa msaada katika klabu hiyo ya kaskazini mwa London tangu atue klabuni hapo akitokea Barcelona kwa ada ya £35m.

Flamini amesema ``Sanchez ana kila dalili ya kufanya vizuri kama Henry na Robin ambao kwa pamoja wameifungia Arsenal mabao 360.Sitazami magoli yake pekee bali pia nguvu anayoitumia katika kuisaidia timu.

Sanchez amekuwa akipambana sana.Ni mtu anayechukia kushindwa hivyo sitoshangaa akifikia mafanikio ya watangulizi wake Henry na Robin"alimaliza Flamini

Arsenal iko nafasi ya tano katika msimamo wa ligi nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea kwa pointi nane.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: FLAMINI:SANCHEZ KAMA THIERRY HENRY Rating: 5 Reviewed By: Unknown