Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti kuhusu hali ya mgongano kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na Bodi ya ligi Tanzania (Tanzania Premier league Board).
Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
1.Bodi ya
ligi imeundwa kwa mujibu wa Katiba ya TFF kifungu 40(11).Hivyo Bodi ya ligi ni
zao la Mkutano Mkuu wa TFF.
2.Katiba ya
TFF imeipa mamlaka kamati ya utendaji ya TFF kutunga kanuni za uendeshaji wa
Bodi ya ligi,kanuni hizi ndiyo nguzo kuu ya uendeshaji wa shughuli za Bodi ya
ligi na ndizo zinaipa Bodi uhalali wake wa
kuendesha shughuli zake za kila siku.
kuendesha shughuli zake za kila siku.
3.Bodi ya
ligi ni chombo cha TFF kama vilivyo vyombo vingine vikiwemo kamati mbali mbali
za TFF.Kisheria Bodi ya ligi sio chombo huru (its not a legal entity) hivyo
Bodi pamoja na mambo mengine haina mamlaka ya kuingia mikataba ya aina yoyote
ya kisheria .
4.Katiba ya
TFF inatamka kuwa Bodi ya ligi itaheshimu na kufuata maagizo ya TFF.Maagizo
haya yanatolewa na Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya kamati ya utendaji ya TFF.
5.Mwenye
mamlaka ya kutengua maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF ni Mkutano Mkuu wa TFF
peke yake,hakuna chombo kingine cha chini chenye mamlaka hayo.
6.Kanuni za
mashindano zinaandaliwa na kamati ya mashindano ya TFF na kupitishwa na kamati
ya utendaji ya TFF. Kikao cha kamati ya utendaji kilichopitisha rasimu ya
kanuni za ligi za mwaka 2014/15 kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa bodi ya
ligi,Makamu mwenyekiti wa Bodi ya ligi na pia Mwenyekiti wa kamati ya
mashindano ya TFF,hawa wote ni wajumbe wa Bodi ya ligi na walishiriki
kikamilifu katika kikao cha kamati ya utendaji kilichopitisha kanuni za ligi
2014/15 ukiwemo na utaratibu wa mgawanyo wa mapato ya milangoni na ya
udhamini.Katiba ya TFF inaagiza hivyo kuwa Viongozi wakuu wa Bodi ya ligi
watakuwa pia ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF. Aidha mtendaji mkuu wa
Bodi ya ligi alikuwepo kwenye kikao hiki cha kamati ya utendaji kama mwajiriwa.
7. Uamuzi wa
kuunda mfuko maalum wa kuendeleza soka la vijana ni uamuzi uliopitishwa na kamati
ya utendaji.Lengo la kuanzishwa mfuko huu ni kuwa na chombo maalum ambacho
kitakuwa kinakusanya fedha toka vyanzo mbali mbali kwa ajili ya kuendeleza
miradi ya soka la vijana nchini.Kwa sasa miradi hii ni:
(a)
Kuanzisha vituo vya kulea na kuendeleza vipaji vya watoto kuanzia miaka 8-17
(sports centres) katika kila mkoa nchini mwetu.Mradi huu ni mkubwa utahitaji
nyenzo hasa walimu na vifaa.
(b) Kuandaa
timu ya taifa umri chini ya miaka 12 kwa ajili ya mashindano ya Afrika umri
chini ya miaka 17 mwaka 2019. Timu hii itaanza kuandaliwa mwaka huu Desemba
baada ya mashindano ya kitaifa umri chini ya miaka 12. Hii timu itakusanywa na
kuwekwa katika shule moja ya bweni ambapo watalelewa na kuendelezwa vipaji vyao
wakiwa pamoja huku wanasoma.Tanzania tumeomba kuwa wenyeji wa fainali hizi.
(c) Kuandaa
timu ya Taifa umri chini ya miaka 14 kwa ajili ya michuano ya awali mwaka 2016
kuelekea fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2017.
(d) Kuandaa
timu ya Taifa umri chini ya miaka 17 kwa ajili ya michuano ya awali mwaka 2016
kuelekea fainali za Afrika umri chini ya miaka 20 mwaka 2017.
(e) Kuandaa
mashindano ya Taifa ya mpira wa wanawake na ligi ya taifa ya mpira wa wanawake.
Miradi yote
hii muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania haina udhamini lakini ni
lazima ifanyike ili tujihakikishie tunainua mpira nchini mwetu.Mafanikio ya
miradi hii sio tu yatafaidisha na kuimarisha timu zetu za Taifa lakini pia
yatakuwa chimbuko madhubuti la wachezaji mahiri wa vilabu vyetu vya mpira wa
miguu.
Kimsingi tunatarajia
kuwa vyanzo vikuu vya mapato ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya mpira Tanzania
vitakuwa:
– Mapato
yatokanayo na mechi za ligi zetu madaraja yote
– Mapato
yatokanayo na mechi za kimataifa
– Wadhamini
– Serikali
kuu kupitia bajeti za Wizara zenye dhamana ya michezo,halmashauri na vyuo
– Wafadhili
– Shughuli
mbali mbali za kutunisha mfuko.
Kamati ya
utendaji ya TFF ilimteua Bwana Leodeger Tenga kuwa mwenyekiti wa kwanza wa
mfuko huu na wajumbe wake ni Bw Tarimba Abbas, Bw Ephraim Mafuru, Mzee Ayoub
Chamshama Bw Frederick Mwakalebela na Mh Zarina Madabida. Bw Henry Tandau na Bw
Boniface Wambura ni waratibu wa mfuko huu. Imani ya TFF ni kuwa wajumbe hawa
kwa kutumia uzoefu wao katika uongozi wa jamii watatusaidia kuhakikisha mfuko
huu unaanza vyema shughuli zake.
Upande wa
TFF tumefungua akaunti maalum benki kwa ajili ya kuingiza fedha zote
zinazokusanywa kama mchango wa TFF kwenye mfuko huu zikiwemo asilimia 5 za
makato ya fedha za udhamini na ZILE zitokanazo na mfuko wa jichangie,TFF inatoa
wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu Tanzania kuchangia mfuko huu ili utumike
kunusuru mpira wetu. Fedha zitakazokusanywa matumizi yake yatasimamiwa na
kanuni za uendeshwaji wa mfuko huu.
Hitimisho:
Kila
mwanafamilia wa TFF anawajibika kuheshimu na kufuata maelekezo ya Kanuni za
mashindano ya ligi kuu kama zilivyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF .Hivyo
utaratibu wa mgawanyo wa mapato yatokanayo na fedha za milangoni na za
wadhamini kama ulivyoainishwa kwenye kanuni hizi uko pale pale. Ninaiagiza Bodi
ya ligi kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya utendaji ya TFF mara
moja. Mwenye malalamiko kuhusu kanuni hizi ayalete kwenye vyombo husika vya TFF
kwa kufuata Katiba,kanuni na taratibu za Shirikisho.Sote tunajenga nyumba moja
hakuna haja ya kugombea fito.
0 comments:
Post a Comment