Gary Neville anapaswa kuondelewa kuwa
kocha wa England na nafasi hiyo akapewa Sol Campbell,hiyo ni kwa mujibu wa Campbell
mwenyewe.
Campbell
ambaye ameichezea timu ya taifa ya England michezo 73 na kufunga goli moja kati ya mwaka 1996 na
2007 anaona Neville ambaye ameichezea timu hiyo michezo 85 bila ya kufunga goli lolote kati ya mwaka 1995
mpaka 2007 anapaswa kuondolewa katika nafasi yake ya ukocha msaidizi katika
timu ya taifa ya England.Campbell na Neville wameitumikia klabu hiyo kwa miaka 11.
Akijibu
swali aliloulizwa na shabiki mmoja wa soka katika tamasha la Cheltenham
Literature Festival ni nini kifanyike ili timu hiyo iache kufungwa magoli ya
ajabu ajabu (mengi) Campbell alijibu
“Mwondoeni Gary Neville na nafasi
hiyo mnipe mimi kwa kuwa nina sifa zote.Najua nini cha kufanya ili vijana
wafanye vizuri”
Mpaka sasa
England hawajaruhusu goli lolote lile katika michezo yake minne tangu
ilipoondolewa kwa aibu katika fainali za kombe la dunia kwa kupokea vichapo
toka kwa Italia na Uruguayi.
Wakati
Neville akiwa na leseni A na B inayotambuliwa na UEFA,Campbell aliendelea
kujinadi
“Kwa sasa nafanya mafunzo ya ukocha
yanayotambuliwa na chama cha soka cha Walace.Niko katika mwaka wa mwisho wa
mafunzo.Kama sitopata kazi kufundisha hapa ndani ya miaka michache nitaangalia
sehemu nyingine pia.
0 comments:
Post a Comment