728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 15, 2014

    TALISCA AZIDI KUWACHONGANISHA WENGER NA MOURINHO

    Klabu ya Arsenal inapanga kutoa kitita cha £8m ili kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Celtic ya Scotland Muholanzi Virgil van Dijk mwezi januari.

    Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuipiku klabu ya Chelsea na kukalia kiti cha uongozi katika mbio za kumnasa mshambuliaji hatari wa klabu ya Benfica Mbrazil Anderson Talisca mwenye thamani ya £17m.

    Klabu ya Aston Villa inapanga kumpa mkataba mpya kiungo wake kinda Jack Grealish ili kuzima jaribio la klabu ya Chelsea kumsajili mwezi januari.

    Klabu ya Real Madrid imeongeza mbio za kumuwania mlinda mlango asiye na furaha katika klabu ya Chelsea Peter Cech (31) ili kujiimarisha katika mbio za kuusaka ubingwa wa ligi ya La Liga.

    Mshambuliaji wa klabu ya Westham Muingereza Andy Carroll amesema hana mpango wa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Newcastle hivi karibuni licha ya kutokuwa na namba ya kudumu katika klabu hiyo ya London

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TALISCA AZIDI KUWACHONGANISHA WENGER NA MOURINHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top